﻿KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
"Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote;"
Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu;
Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo.
"Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada."
"Tuongoe njia iliyo nyooka,"
"Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea."
